Friday , 15th Jun , 2018

Msanii wa Bongo Flava Dully Sykes, amesema muziki unamiiko yake ambayo kila msanii anapaswa kuifuata ili aweze kuishi kwenye muziki muda mrefu na kujipatia heshima kubwa kupitia kazi yake.

Akizungumza na www.eatv, Dully ameeleza kuwa wasanii wengi wazamani waliokuja kabla na baada yake katika tasinia ya muziki walishindwa kuheshimu miiko ya muziki kitu ambacho kimewapelekea wao kushindwa kupata maendeleo na hata kutimiza malengo yao.

Dully ameitaja miiko hiyo ni pamoja na msanii kujihehimu, kuheshimu wale wanaomsaidia katika kufikia malengo yake, na pia kuheshimu kile alichochagua kukifanya kwani ndio ajira yake.

Dully aliendelea kusema kuwa muziki unabadilika kila wakati, na pia kila kukicha wanazaliwa wasanii wapya hivyo ni lazima msanii awe na ubunifu wa hali ya juu ili aweze kuendelea kufanya vizuri katika soko la muziki.

“Mara nyingi watu hawaelewi muziki unamiiko na ukiifuata  unaweza kukaa kwenye muziki muda mrefu, ila ukiivunja miiko hiyo huwezi kufika” alisema Dully.

Hivi sasa Dully Sykes anatamba na wimbo wake mpya wa Zoom ambao ameupindua kutoka katika wimbo wa Dr. Dre na LL Cool J wenye jina kama la wimbo wake.