msanii wa muziki wa Uganda Desire Luzinda
Desire ambaye picha zake za utupu zimeweza kumpatia wakati mgumu sana hasa mbele ya hadhara, amewashukuru mashabiki hawa kwa kutoa shangwe kama ambavyo wangefanya kwa mtumbuizaji mwingine yoyote yule, licha ya wakati mgumu na wa aibu ambao amepitia.
Katika onesho hili la Desire mwishoni mwa wiki, shangwe za mashabiki ziliambatana na jitihada za kutaka kumsogelea karibu zaidi, malengo yao yakihisiwa kuwa ni kutaka kuhakikisha vile walivyoviona katika picha kwa uhalisia zaidi, huku wengine wakitafsiri kuwa hatua hii ilikuwa ni kuonesha upendo tu.