Tuesday , 13th Dec , 2016

Msanii nguli wa muziki kutoka nchini Keny mwanadada Wahu ameeleza jinsi elimu yake ya shahada hisabati aliyoipata katika chuo kikuu cha Nairobi, inavyomsaidia katika shughuli zake za muziki.

Wahu akiwa katika jukwaa la EATV Award

Wahu ametoa kauli hiyo alipokuwa kwenye usiku wa EATV Awards akiwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza na vilevile kutoa tuzo kwa washindi.

Alisema yeye anapenda kusoma kwa ajili ya kuwa na mpango mbadala wa maisha, na kwamba shahada yake ya hisabati inamsaidia mengi ikiwemo kuhesabu pesa.

Wahu ambaye pia ana shahada ya uzamili (Masters) ya mawasiliano ametoa ushauri kwa wasanii wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, kuhusu mbinu za kuusukuma muziki wa ukanda huo mbele zaidi.

Mtazame hapa:- 

Tags: