Monday , 30th Nov , 2015

Nyota wa muziki Dyna Nyange, katika kuhamasisha pia wasichana wengine ameeleza kuwa, mbali na muziki, maisha yake yanaendeshwa na kipato kinachotokana na biashara zake ambazo amezianzisha.

Nyota wa muziki nchini Dyna Nyange

Mkali huyo wa kibao cha 'I Do' ameelezea kuwa biashara hizo ni zile ambazo huziendesha kwa kutumia watu ama wadau wake wa karibu ambao huwekeza pesa zake kwao.

Dyna amesema kuwa, anatumia utaratibu huo na malipo yake hufanyika kila wiki licha ya kutotaka kuingia ndani zaidi kuweka bayana ni biashara gani hasa, staa huyu akiwa ni moja kati ya wanadada wanaoishi maisha ya juu kabisa hapa mjini.

Kuhusiana na anapozichanga pesa zake, Dyna hapa anaeleza zaidi.