Tuesday , 23rd Jun , 2015

Staa wa muziki Daddy Owen kutoka nchini Kenya, ameonesha kuguswa na tukio la moto kuteketeza soko la Gikomba hii leo huko Nairobi, hii ikiwa si mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea.

Daddy Owen

Daddy Owen sambamba na kuelezea masikitiko yake, ameweka wazi kuwa pia binafsi amewahi kuwa na kibanda katika soko hilo kabla ya kuingia katika muziki, na hawezi kusahau maisha ya wasi wasi kila siku katika eneo hilo.

Staa huyo ametaka jitihada kufanyika kuepusha ajali kama hizo, hali halisi ya msongamano katika soko hilo ikitajwa kuwa chanzo kikubwa cha madhara makubwa wakati wowote dharura inapotokea.