Thursday , 2nd Jul , 2015

Kuchelewa kwa kolabo ya nyota wa Bongofleva, Bob Junior na star wa muziki wa nchini Uganda Jose Chameleone ambayo amewaahidi mashabiki wake kwa muda mrefu, imeanza kumtesa mkali huyo kutokana na kuwa na hofu ya kutoa rekodi nyingine.

Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania Bob Junior

Bob Junior amesema kuwa ana rekodi nyingine kali sana, ikiwepo albam ambayo anatarajia kuiita 'Ukweli Wangu', akiwa sasa hawezi kutoka na rekodi nyingine baada ya kufungwa na ahadi aliyoiweka.