Tuesday , 29th Dec , 2015

Tukiwa ndio tunauaga mwaka 2015 kuelekea 2016 baadhi ya wasanii wa muziki wameelezea mafanikio yao katika tasnia ya burudani ambapo star Belle 9 amekiri kuwa amepiga hatua baada ya menejimenti yake ya Vitamin Music kumsapoti kwa nguvu zote.

staa wa muziki nchini Belle 9

Belle 9 ambaye ametamba na video ya funga mwaka iliyobatizwa jina 'Shauri Zao' ameongea na enewz kuwa project yake ya Burger movie Selfie pia imemfungulia pazia na anaamini kuwa mwakani atazidi kutoa kazi nyingine kali huku akivishukuru vyombo vya habari na wadau kwa sapoti zao.