Friday , 21st Aug , 2015

Star wa muziki Belle 9 amesema kuwa hivi sasa nafasi yake ya muziki imechukuliwa mno na masuala ya siasa hivyo imekuwa ni vigumu kwake kutoa kazi mpya na amekiri sasa si wakati wake mzuri kutoa ngoma hadi hapo baadaye.

Staa wa muziki Belle 9

Belle 9 amesema pia kuwa hivi sasa anaandaa kichupa cha wimbo wake mpya 'Shauri Zao' huku akiendelea kufanya project zake nyingine ambazo kwa sasa zitaendelea taratibu kutokana na upepo wa siasa kuchukua nafasi kubwa nchini.

Aidha, Belle 9 pia amegusia kuwa hapendi na wala hana hobby kuhusiana na masuala ya siasa na kuweka wazi kuwa anampa pongezi zake Prof Jay katika harakati zake katika muziki wake na siasa kwa ujumla.