Monday , 8th May , 2017

Msanii wa miondoko ya 'Hip hop' Lord Eyez amefunguka mazito kwa kudai yeye hajawahi kusainiwa wala kusimamiwi kazi zake za muziki na 'Label' ya BANA inayomilikiwa na Baraka the Prince pamoja na mpenzi wake Naj kama mwenyewe anavyojitangazia.

Msanii wa'Hip hop' Lord Eyez

Lord Eyez amebainisha hayo baada ya kuenea zile tetesi za muda mrefu zikiaminisha watu kuwa msanii Baraka the Prince ameweza kumrudisha katika soko la muziki mkongwe huyo wa rapu kwa kumsainisha ndani ya 'Label' yake.

"Watu wanaongea vitu ambavyo hawavijui..kwasababu mimi sisimamiwi na Baraka wala sijasainiwa na Baraka. Kwa sababu Lord Eyez kusainiwa inahitaji 'Label' yenye nguvu kweli kuweza kunisaini". Alisema Lord

Katika hatua nyingine, Lord amewasii vijana wa sasa kuacha kabisa kutaka kujaribu ama kuonja madawa ya kulevya kwa kuwa zinaangamiza maisha na ukiingia katika dimbwi hilo kutoka siyo rahisi.

"Madawa yana nuksi utaona mambo yako hayaendi yanasusua tu...Dawa za kulevya zimekuwa shinda hasa kwa vijana wengi wanateketea..Nawaambia dawa za kulevya hazijaribi, usiguse, usinuse, usitumie dawa za kulevya kwa sababu ni hatari zitakuangamiza". Alisisitizia Lord