Wednesday , 24th Jun , 2015

Kufuatia taarifa za uvumi wa kifo cha star wa miondoko ya dansi, Banza Stone kutapakaa kuanzia jana usiku, hii ikiwa si mara ya kwanza kwa kitendo kama hiki kutokea, nyota huyo ameongea na eNewz binafsi kuwahakikishia mashabiki wake kuwa yupo hai.

Banza Stone

Akionesha kukerwa na habari hizo za kuzushiwa kifo mara kwa mara, Banza Stone kwa maneno yake mwenyewe ameeleza kuwa yupo sawa kama anavyosikika mwenyewe hapa, ambapo tuliongea naye akiwa anafurahia mlo wake wa tunda la parachichi mapema hii leo.