Tuesday , 2nd Dec , 2014

Kampeni ya kuwatetea wanawake kuvaa nguo vile wanavyojisikia, imeendelea kuungwa mkono na watu maarufu huko nchini Kenya, safari hii rapa Bamboo naye akiweka maoni yake wazi kuwa watu ambao huwavamia wanawake waliovaa vibaya na kuwavua nguo.

msanii wa muziki nchini Kenya Bamboo akiwa na dada yake Victoria Kimani

Rapa huyu amesema kuwa, wanaume wanaovamia wanawake hao na kuwavua nguo ni wanyama, wakatili na wanachostahili ni kifungo tu bila kujali ni kwa namna gani mwanamke waliomvamia amevaa.

Kampeni hizi zimejizolea umaarufu nchini Kenya hasa baada ya makundi ya wanaume kuibuka na kushirikiana kuwavamia wanawake waliokuwa wamevaa nguo fupi na kuwavua nguo katika matukio matatu tofauti nchini humo.