Saturday , 9th Aug , 2014

Rapa Baghdad ambaye kwa sasa anafanya kazi zake za muziki akiwa na Clique ya Vipaji TZ, amesema kuwa, project yake mpya ya Haters, ni moja kati ya kazi kubwa kabisa kwake kuwahi kufanya tokea ameanza muziki.

Baghdad

Rapa huyu ambaye muonekano wake umebadilika kutoka kwenye u BIG hadi kwenye U Slim Shady ndani ya kipindi kifupi, amesema kuwa project ya Haters ameifanya pia katika matoleo mbalimbali na kushirikisha wasanii wakubwa na wadogo, na hivi karibuni ataziachia kwa mashabiki wake.

Baghdad amesema kuwa, baada ya kukamilisha video ya kazi hizi kutoka kwa Adam Juma, ataanza kuachia matoleo mengine ya kazi hii, ambapo ndani yake watakuwa wamehusika pia wakali kama vile rapa Proffesa Jay, Mwana FA, Young Killer, Chibwa na wasanii wengine wa rika tofauti.