Monday , 7th Sep , 2015

Nyota wa muziki AT ambaye anatikisa chati sasa kupitia project mpya ya Mama Mie, ameweka wazi mpango wake mkubwa wa kuwania nafasi ya kisiasa.

Nyota wa muziki AT

AT ameahidi kutumia mkakati utakaotumia akili ndogo na maarifa makubwa kuhakikisha kuwa hakosi nafasi hiyo kama wasanii wenzake wengi katika mbio za kisiasa mwaka huu.

Star huyo amesema kuwa, wasanii wenzake walikurupuka na kuangukia pua, yeye binafsi akitaka mashabiki kushika maneno yake na kumbana baada ya miaka 5 juu ya mpango wake huo wa kushika nafasi ya kisiasa ambao hakuna atakayeamini.