Monday , 27th Oct , 2014

Mkali wa michano ya Hip Hop kutokea Nairobi Kenya, Abbas Kubaff anatarajia kuwa baba kati ya mwishoni mwa mwaka huu ama mwanzoni mwa mwaka ujao kutoka kwa mpenzi wake Pam Curtis.

Abbas Kubaff mwenyewe akiwa mwenye furaha amethibitisha taarifa hizi, huku akiweka wazi kuwa mpango wa kuhalalisha mahusiano yao utafikiriwa baada ya mtoto kuzaliwa.

Abbas kwa sasa anaonekana mwenye furaha akiwa ametulia katika mahusiano yake haya mapya baada ya misukosuko mingi kutoka katika mahusiano yake yaliyopita.