Sunday , 8th Jul , 2018

Muigizaji Wema Sepetu ameweka wazi hisia zake na kusisitiza juu ya umuhimu wa kuwepo kwa hali ya amani katika kipindi hiki cha msiba wa mtoto wa Patrick.

Migizajia Wema Sepetu kushoto akiwa na Muna Love

Akizungumza hayo kwenye viwanja vya Leaders kinondoni ambapo mwili wa mtoto ulikua unaagwa, Wema amefunguka juu ya sintofahamu iliyoleta mijadala isiyoisha mitandaoni inayompa wakati mgumu Muna Love ambaye ni mama wa marehemu mtoto Patrick.

“Kuhusu mitandao naomba tuyaache yabaki mitandoni ninaimani mtoto wenu atakua na furaha zaidi akiona kuna upendo kati yenu na sio huu mgawanyiko ambao unaendelea, Muna unajua nakupenda na nitaendelea kukupenda yaliyopita si ndwele tugange yajayo”. Alisema Wema.

Aidha Muigizaji Wema hakusita kutoa maneno ya kumpa moyo mama wa mtoto Patrick (Muna), juu ya msiba mzito wa mwanaye uliomfika.

Mimi sijabahatika kupata mtoto lakini naelewa uchungu anaopitia Muna. Siwezi kusema naelewa kwa ukubwa kwa sababu sijui uchungu wa mwana lakini nina theluthi ya ufahamu kwa kiasi gani Muna anaumia" .

"Najua hakuna mzazi anayependa kumzika mwanaye, mama yangu huwa ananiambia ni bora zaidi mtoto kumzika mzazi, hivyo naamini Mungu atawapa nguvu.” Amesema Wema Sepetu.