Thursday , 8th Jan , 2015

Jumla ya watu 284 hawana mahali pa kuishi wilayani Kongwa Mkoani Dodoma, kufuatia nyumba zao zipatazo 46 kubomolewa na mafuriko makubwa yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapa.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Alfred Msovella akimuongoza aliekua Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi wakati akikagua ujenzi wa ndani wa nyumba za shirika la nyumba .

Akizungumza na East Africa Radio, Mkuu wa Wilaya ya kongwa, Alfred Msovella amesema mafuriko hayo yametokea katika vitongoji viwili vya Wezamtima na Chang’ombe vilivyoko Wilayani humo.

Amesema mafuriko hayo yamesababishwa na mvua zilizonyesha kati ya Desemba 29 na 31 mwaka jana ambapo amesema mafuriko hayo yalisababsiah madhara makubwa.

Aidha Mkurugenzi huyo amesema tukio hilo limetokea katika vitongoji viwili tofauti ambapo katika kitongoji cha mwezamtima kijiji cha mlanje jumla ya kaya 36 na wakazi 227 walikosa makazi huku kitongoji chengine cha Changombe katika kijiji hicho jumla ya kaya 10 na wakazi 57 walikosa makazi.

Msovela amesema kuwa serikali ya mkoa wake imeshakua hatua kwa kiwangi kikubwa kwa kuweza kuwahamisha wananchi kutoka mabondeni na kuwapeleka sehemu za muiniko lakini pia serikali imetoa msaada kwa wahanga kuweza kujikimu kwa sasa.