Monday , 13th Apr , 2015

Naibu wazira wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Kebwe Stephen Kebwe ameelezea kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na kampuni ya bia nchini - TBL katika uzalishaji wa bidhaa zake zikiwemo bia.

Dk Kebwe amesema hayo leo wakati alipokitembelea kiwanda hicho kilichopo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa wizara yake wa kutembelea maeneo yaliyo chini ya usimamizi wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Naibu Waziri Kebwe amesema malengo ya mwaka huu ni kufanya usimamizi katika maeneo yanayotoa huduma kwa wananchi ikiwemo viwanda, na kuongeza kuwa ni lazima viwanda vizalishe kulingana na viwango vinavyotakiwa kisheria na kwamba wizara yake haitokaa na kusubiri ripoti za mezani bali wanatembelea maeneo yaliyo chini yao ili kujihakikishia kuhusu suala la viwango.