Msemaji wa WHO Christian Lindmeier
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Msemaji wa WHO Christian Lindmeier ameeleza kwamba kirusi chenyewe cha Zika si hatari, kwani husababisha ukurutu mwilini.
Hata hivyo ameeleza kwamba Brazil imeshuhudia pia visa 4,000 vya watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo, miongoni mwao 49 wakiwa wamefariki dunia, ikidaiwa hali hiyo kuwa na uhusiano na kirusi cha Zika.
Aidha amesema kwamba WHO haijapendekeza wanawake kujikinga dhidi ya kupata mimba, akieleza kwamba suluhu dhidi ya kirusi cha Zika hivi sasa ni kujikinga na mbu aina ya Aedes, ikiwa ni Brazil au kwingineko.