Sunday , 28th Sep , 2014

Waumini wa dini mbali mbali nchini Tanzania wameshauriwa kujenga tabia ya kujitolea damu ili kuweza kuwasaidia wale wenye mahitaji wakiwemo wakina mama wajawazito na watoto kwa lengo la kuokoa maisha yao.

Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Bw. Rajab Mwenda (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hivi karibuni.

Askofu mkuu wa kanisa la waadventista wasabato jimbo la mashariki mwa Tanzania Askofu Mark Malekana ametoa ushauri huo leo jijini Dar es salaam wakati kanisa hilo lilipoandaa tamasha ka uiambaji na huduma kwa jamii na kushirikisha madhehebu ya dini mbali mbali hapa nchini lengo likiwa ni kusaidia uchangiaji damu kwa hiari.

Wakati huo huo, zaidi ya asilimia 50 ya wagonjwa wanaofika kupima afya zao katika hospital ya Aga Khan jijini Dar es Salaam wamegundulika kuwa na maradhi ya moyo yanayochangiwa na matumizi mabaya ya vyakula, unywaji holela wa pombe pamoja na uvutaji wa sigara.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Dkt. Mustaafa Bapumia wakati hospital hiyo ilipoendesha zoezi la upimaji wa magonjwa ya moyo bure kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam.