Waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma Bi. Celina Kombani.
Hatua hiyo kwa mujibu wa serikali, itasaidia kuepukana na tatizo la muda mrefu ambapo watumishi wengi wa idara na taasisi za umma hususani walimu wamekuwa wakikosa kulipwa mishahara yao kwa wakati kutokana na tofauti ya taarifa wanazoziwasilisha.
Akijibu hoja mbalimbali za wabunge juu ya malipo ya watumishi, Waziri wa nchi ofisi ya rais Menejimenti na Utumishi wa Umma Mhe. Celina Kombani amesema serikali inafanya jitihada kulipa mishara kwa wakati, lakini matatizo madogo madogo mengi yakisababishwa na uzembe au udanganyifu yamekuwa yakiathiri malipo ya watumishi.
Pia Waziri Kombani ameelezea kuwa, maamuzi ya kima cha chini cha mshahara au makato ya PAYE wanayokatwa wafanyakazi ni maamuzi yaliyofikiwa baada ya wizara kukaa na vyama vya wafanyakazi na kukubaliana.