Wednesday , 11th Jun , 2014

Watuhumiwa nane (8) kati ya 16 wanaokabiliwa na kesi ya kuhusika  ulipuaji wa bomu katika baa ya Night Pack Arusha na mtandao wa kigaidi wamepandishwa tena kizimbani katika mahakama kuu  kanda ya Arusha na kusomewa kwa mara ya pili mashtaka.

Watuhumiwa hao wakiondolewa mahakamani

Watuhumiwa nane (8) kati ya 16 wanaokabiliwa  na kesi  ya  kuhusika  ulipuaji  wa  bomu katika   baa   ya Night  Pack  ya  jijini  Arusha  na mtandao   wa   kigaidi   wamepandishwa  tena  kizimbani   katika   mahakama kuu  kanda  ya Arusha na kusomewa kwa mara ya pili mashtaka yanayowakabili. 

Watuhumiwa hao wamesomewa  mashtaka yanayowakabili    mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo   Mustapher Siyani,  akisaidiwa  na wakili wa serikali  Hellen   Rwijag, na  hawakutakiwa kujibu lolote  kuhusiana na  kesi  inayowakabili. 

Hata hivyo  washtakiwa  hao  walimwomba  hakimu   kulitaka  jeshi  la polisi   kuwasilisha  mahakamani   hapo  mali  zao  zilizochukuliwa wakati  wanakamatwa zikiwemo  simu  za  mkononi Nguo  na  Viatu.

Hata  hivyo  habari  kutoka  mahakamani hapo zimeeleza  kuwa  baadhi ya  vitu  wanavyohitaji watuhumiwa   hao  hawawezi kupewa  kutokana  na kuwa  sehemu  ya  ushahidi  wa  kesi inayowakabili .

Wakati  watuhumiwa  hao  wanafikishwa mahakamani  hapo  ndugu  na  jamaa  zao    walifika  kwa   wingi   wakitaka   kuwaona   hali iliyosababisha  askari   kufanya   kazi   ya   ziada   ya   kuwadhibiti   na  kuimarisha  ulinzi.

watuhumiwa hao wanakabiliwa  na   kosa kujihusisha na  usajili, usafirishaji   wa   vijana   kwenda   nje  ya nchi  kwa  ajili ya  kupata mafunzo   ya  uhalifu  na ugaidi  na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 25 mwaka huu itakapotajwa tena.

Kundi  la  pili   la  washitakiwa  wengine  wa  kesi  ya kulipua   bomu   wanatarajiwa   kupandishwa   kizimbani  kesho  tarehe  12/06/14.