Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 40 kwa tuhuma za kula njama za kutoa makontena zaidi ya 2,500 kinyume na utaratibu na kuisababishia hasara serikali ya mabilioni ya fedha.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Suleiman Kova amesema kati ya watuhumiwa hao 26 ni watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, watumishi 3 kutoka bandari Kavu na wengine 11 ni watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA kwa kuhusika na upotevu wa makontena 2,489.
Wakati huo huo, Kamishna Kova amesema jeshi la polisi linawashikilia watuhumiwa wanne kwa kujihusaisha na unyang'anyi wa kutumia silaha katika tukio lililotokea Chanika baada ya watu hao kuvamia Benki na kupora fedha huku meneja wa benki moja wapo akihusika pia.