Monday , 19th Jan , 2015

Zaidi ya watu 200 wanao piga debe katika standi ya mabasi ya mkoa wa singida , wameweka mawe makubwa na kuzuia mabasi zaidi ya 30 yasiendelee na safari zake wakitakai stand hiyo kufanyiwa ukarabati.

Mkuu wa wilaya ya Singida Bi.Queen Mlozi.

Wakieleza kwa jazba mawakala hao pamoja na madereva wamesema wamefikia uamuzi huo baada ya manispaa ya Singida kushindwa kufanya matengenezo katika kituo hicho cha mabasi ambacho kina mitaro mikubwa ambayo ina sababisha mabasi kuharibika, ghuba la taka kujaa na kuhatarisha milipuko ya magonjwa, huku manispaa ina kusanya kila siku zaidi ya shilingi laki sita ikiwa ni ushuru wa mabasi zaidi ya mia tatu yanayo pita na kulala katika standi kuu ya mabasi ya Missuna .

Kwa upande wao Mkurungenzi wa Manispaa ya Singida Bw. Joseph Mchina na Mkuu wa wilaya ya Singida Bi. Queen Mlozi baada ya kufika katika kituo hicho wamekiri kuwepo kwa mitaro mikubwa na wamesema manispaa ya Singida imetenga jumla ya shilingi milioni mbili kufanya ukarabati mdogo wakati wakisubiri fedha kutoka benki ya dunia kuweka lami na kumaliza kabisa tatizo hilo

Katika sakata hilo jeshi la polisi halikuwa mbali pamoja na kikosi kamili cha kuzuia fujo kufika na silaha za moto na mabomu ya machozi, mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Singida Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Bwana Magai Chasa amewahakikishia wananchi na abiria walio kuwa wakisubiri usafiri uvunjifu wa amani hauwezi kutokea.