
Prof. Mkumbo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na EABREAKFAST kuhusiana na taarifa za wanafunzi wengi wa vyuo baadhi kusahau lengo la msingi na kujiingiza kwenye masuala ya mapenzi.
''Mazingira ya chuo kikuuu vijana wanakuwa huru sana na wengi hujiingiza katika mapenzi tafiti zinaonyesha kuwa wanafunzi wanavyoingia vyuo vikuu asilimia 20 mpaka 30 husema wameshafanya mapenzi lakini wanapomaliza asilimia huongezeka na kufikia 80 hadi 90 ''- Amesema Prof. Mkumbo.
Aidha Mhadhiri huyo amesisitiza kuwa jambo ambalo ni la msingi kwa vijana hao ni kuhakikisha wanafanya mapenzi kwa njia salama na wahakikishe hawafanyi mapenzi kwa mashinikizo wawe wameamua wenyewe.
Hata hivyo wanafunzi waliozungumza katika kipindi wamesema kwamba kujiingiza katika mapenzi hutegemea na tabia ya mtu na wengine hufuata mkumbo kwa kuiga namna wengine wanavyofanya huku wengi wakitawaliwa na tamaa za kutaka kuishi maisha ambayo siyo ya kiuhalisia.