Tuesday , 23rd Jun , 2015

Serikali kwa kushirikiana na mradi wa kuimarisha maeneo yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania (Spanest) imewataka wananchi wanaoishi karibu na hifadhi za Taifa kuyalinda maeneo hayo ili yasiharibiwe na majangili.

Haya ni makundi makubwa ya Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa ni hifadhi yenye mvuto mkubwa kwa wageni na watalii wa ndani pia kutembelea hifadhi

Wito huo umetolewa leo na Mratibu wa Mradi huo, Godwell ole Meing’ataki wakati akizungumza na waandishi wa habari wilayani Chamwino mkoani Dodoma na kusema kuwa mradi huo unatekelezwa katika mikoa minne ya Tanzania Bara ambayo ni Mbeya, Iringa, Njombe na Wilaya ya Chamwino iliyoko Mkoani Dodoma.

Meing’ataki amesema kuwa zipo faida nyingi za kuhifadhi maeneo ya hifadhi za wanyapori pamoja na zile za wananchi kwani ni kivutio kikubwa cha utalii wa ndani na nje ya nchi.

Amesema kuwa kuna faida kubwa za kuwalinda wanyama kwani wanaliingizia Taifa fedha nyingi za kigeni.

Kwa upande wake katibu tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Juliana Kilasara amesema kuwa katika Wilaya ya Chamwino mradi huo unatekelezwa katika vijiji vinne vinavyopakana na hifadhi ya Mto Ruaha ambavyo ni kijiji cha Mpwayungu, Manda, Ilangali pamoja na kijiji cha Chilungulu