
Wakiongea na waandishi wa habari leo, baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa eneo lao limepitiwa na mradi wa njia ya umeme kutoka Somanga mpaka Kinyerezi hivyo tangu mwaka 2011 walipewa taarifa ya kuzuiwa kufanya maendeleo yoyote katika eneo hilo.
Wameeleza kuwa Tanesco iliwalazimisha kusaini malipo yao bila hata ya kujua gharama halisi wanazoenda kulipwa kwa madai kuwa endapo watakataa kulipwa kiasi hiko kidogo wanaweza jikuta wanakosa kabisa, kwa hofu wananchi waliamua kuchukua kiasi hiko kidogo cha pesa na baadaye wakafungua kesi, na mahakama ikawataka Tanesco warudi kufanya tathmini upya.
Tatizo la uelewa mdogo wa masuala ya sheria linaonekana kupelekea kuwanyima haki wananchi wengi na kujikuta wakiingia makubaliano bila kuwa na taarifa muhimu hivyo kuleta mgogoro wa kimaslahi hapo baadae.
