Wednesday , 23rd Mar , 2016

Jamii Mkoani Arusha imetakiwa kuachana na dhana potofu ya matumizi ya gongo kama tiba kipindupindu na badala yake kuzingatia kanuni za afya ili kuondokana na maambukizi ya ugonjwa huo ambao katika kipindi kirefu umekuwa ukiripotiwa katika mikoa ming

Mgambo wa jiji akimwaga pombe za kienyeji aina ya Gongo zilizokutwa kwenye nyumba za wakazi wa Mtaa wa Matejo jijini Arusha

Wito huo umetolewa kufuatia uchunguzi uliofanywa na wanahabari Mkoani Arusha na kubaini kuwa, baadhi ya wakazi wa Kata ya Ngarenaro jijini Arusha wamekuwa wakitumia gongo kama tiba bila kujali athari zinazotokana na matumizi ya ya pombe hiyo haramu.

Baadhi ya wakazi hao akiwemo Bi. Maria Shayo ambae ni mzazi wa mwezi mmoja licha ya kutopima na kubaini tatizo amesema yeye na motto wake wa mwezi mmoja waliugua na kupona huku majirani wakishuhudia.

Nao baadhi ya watumiaji pombe hiyo akiwepo Akida Samweli wameiomba serikali kufanya utafiti wa pombe hiyo kwani wamekuwa wakitumia kama tiba ya magonjwa mbalimbali tangu utoto wao bila kusumbuliwa na maradhi.

Akiongea kwa masharti ya kutokurekodiwa moja ya mpishi wa pombe hiyo amesema wamekuwa wa kichanganya vitu vingi vikali jambo ambalo wanaamini mdudu wa kila aina ya ugonjwa hawezi kustaimili mwilini mwa mtumiaji .

Kufuatia maelezo hayo kituo hiki kilimtafua Mganga Mfawidhi wa jiji la Arusha, Dkt.Jafept Kivuyo kwa njia ya simu akiwa nje ya jiji kikazi ,ambae licha ya kukanusha madai hayo aliwataka wakazi wa jiji kuondokana na imani potofu na kuacha na na matumizi ya pombe hiyo hatari huku akielezea athari za pombe hiyo.

Pamoja na ushuhuda ya pombe kutibu kipindupindu hakuna aliyekiri kupima na kubaini kuwa na kipindupindu.