Sunday , 10th Apr , 2016

Watanzania wametakiwa kuweka wazi vyeti vyao vya wanahisa ili wanapofariki waliowaachia urithi waweze kulithi hisa zao ambazo nyingi zimekuwa zikipotelea katika makampuni yenye hisa.

Mwezeshaji wa semina ya wanahisa kutoka makao makuu ya CRDB, Dar es Salaam, Ngeleja mcharo.

Imedaiwa kuwa Wananchi wengi wamekuwa wakificha vyeti vya umiliki wa hisa na kusababisha wanapofariki ndugu zao kutojua kama walikuwa wakimiki hisa na kupotelea katika makampuni mbalimbali yanayo milikiwa kwa kuuza hisa huku elimu ikidaiwa kuwa ni tatizo.

Hayo yamebainishwa na afisa wa benki yaCRDB Bank, kutoka makao makuu, Ngeleja Mcharo, wakati wa semina ya siku moja ya wanahisa iliyofanyika mjini Njombe.

Meneia waCRDB Bank, tawi la Njombe, Alson Andrew amesema kuwa anatamani sana wateja wengi wangekuwa ni wamiliki wa hisa lakini changamoto kubwa ni suala la elimu kwa wananchi.

Aidha wanahisa wengi wamekuwa wakishindwa kuchukua gawio kutokana na elimu ndogo huku wanahisa wengine wakiwa wamefariki bila kuwaachia warithi kumbukumbu zao.