Saturday , 30th May , 2015

Wanafunzi wa kitivo cha elimu katika chuo kikuu cha Dodoma wameipindua serikali ya wanafunzi wa kitivo hicho kwa madai ya kutowajibika kwa viongozi pamoja na madai ya ubadhirifu wa fedha.

Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM).

Mapinduzi hayo yamefanyika leo asubuhi ambapo wanafunzi hao wamempindua aliyekuwa Rais wa kitivo hicho, John Nzilanyingi na kumuweka aliyekuwa waziri wa afya na mikopo, Simon Mpandalume kuwa Rais wa mpito wa serikali hiyo hadi hapo uchaguzi mkuu utakapofanyika Juni mosi mwaka huu.

Rais aliyepinduliwa anadaiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kuwakandamiza wanafunzi wenzake kwa kushirikiana na uongozi wa chuo.

Aidha anatuhumiwa kwa ufujaji wa fedha za wanafunzi ambapo anadaiwa kutumia sh milion 7 za michango ya wanafunzi kununulia gari yake ya kutembelea.

Mpaka sasa Rais huyo hajulikani alipo kwani baada ya kupinduliwa alitoweka eneo la chuo.