
Agizo hilo limetolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe na Mkuu wa wilaya ya Ludewa, Anatory Choya, wakati akizindua wiki ya unywaji wa maziwa kitaifa ambayo inaadhimishwa mkoani Njombe kitaifa wakati kukiwa na asilimia 52 ya udumavu mkoani humo.
Ameongeza kuwa serikali kama itataka kila shule kuwa na maziwa kama halmashauri hazita weza kifedha basi zianzishe miradi ya ufugaji wa ng’ombe mashuleni.
Katika maadhimisho hayo Ofisa Mifugo Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Abdallah Temba amesema selikali inasambaza madume Bora ya Ngombe ya Mbegu ili kuwasaidia wafugaji kupata Ng’ombe wa Mbegu kwa urahisi.
Mbali na hayo, Zena Issa Ofisa Viwango wa Shirika la Viwango Nchini TBS na Debora Haule Afisa Masoko TBS wanasema wameshiriki maadhimisho hayo ili kutoa elimu kwa jamii ili kutumia bidhaa zilizo sindikwa na kuthibitishwa na shiriki la viwango nchini TBS.