Tuesday , 19th Jan , 2016

Zaidi ya watu 165 wamekamatwa kwa kuishi nchini kinyume cha sheria katika kipindi cha mwaka 2015 kutoka nchi mbalimbali za Burundi,Rwanda, Kenya, Kongo, Mali, Chile, Ethiopia, Naigeria na Zambia.

Zaidi ya watu 165 wamekamatwa kwa kuishi nchini kinyume cha sheria katika kipindi cha mwaka 2015 kutoka nchi mbalimbali za Burundi,Rwanda, Kenya, Kongo, Mali, Chile, Ethiopia, Naigeria na Zambia.

Miongoni mwao, wapo wanaotumikia kifungo nchini huku wengine wakipewa adhabu na kurudishwa makwao
Hayo yameelezwa na Naibu Kamishna wa Uhamiaji, ANDRWE KALEMBO, wakati akizungumzia Operesheni ya kusaka wanaoishi kinyume cha sheria mkoani Tabora ambapo kwa mwaka huu ,amesema wamekamata watu 12,wawili raia wa Uganda ambao wamefukuzwa nchini huku waliobaki wakihojiwa kuhusu uraia wao.

Watumishi wa uhamiaji wanasema wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ya lugha wakati wanapowakamata watu wanaoingia nchini kinyume cha sheria.

Akitoa maoni yake mkazi wa Tabora, MIRAMBO BANDORA, anasema watanzania ni watu wakarimu na ndio maana hawaoni tatizo kwa raia kutoka nje ya nchi lakini amewataka wafuate sheria na taratibu zilizopo, huku ADREW KALEMBO akiwataka wakazi wa Tabora kutoa ushirikiano kuwafichua wanaoishi kinyume na utaratibu.

Mkoa wa Tabora unakabiliwa na changamoto ya kuwa na wahamiaji kwa vile Mkoa wa Kigoma unapakana na nchi jirani za Kongo, Rwanda na Burundi ambao ni jirani na mkoa a Tabora.

Naibu Kamishna wa Uhamiaji, ANDRWE KALEMBO