Wednesday , 1st Jul , 2015

Wanachama mbalimbali wa CCM wameendelea kurudisha fomu zao za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais ambapo kwa siku ya leo jumla ya wanachama nane walitarajiwa kurudisha fomu zao.

Nembo ya Chama cha Mapinduzi.

Miongoni mwa waliorudisha fomu hizo kwa siku ya leo ni waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Waziri wa Maliasili na utalii, Lazaro Nyalandu, Naibu waziri wa fedha Mwigulu Nchemba na Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba.

Wengine ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk, Asha Rose Migiro, Balozi Hassy Kitine, Mbunge wa Nzega, Dk, Hamisi Kigwangala na Malik Marupu.

Mpaka kufikia jioni ya leo jumla ya wanachama 31 walitarajiwa kuwa wamerudisha fomu zao kati ya wanachama 42 waliochukua fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kugombea nafasi ya urais huku ikiwa imebaki siku moja tu ya kukamilisha zoezi hilo.