Friday , 25th Nov , 2016

Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kimewaomba wawekezaji kutoka nchini China kuja kuwekeza viwanda vyao hapa nchini hususani vile vinavyotumia teknolojia rahisi na vinavyoajiri idadi kubwa ya watu katika uzalishaji.

Baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchini China na wanaofanya biashara hapa nchini wakiwa katikia mkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Mapato nchini TRA

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw. Clifford Tandari ametoa wito huo leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano ambao Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imekutana na wafanyabiashara zaidi ya 200 kutoka nchini China wanaofanya biashara zao hapa nchini.

Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Huduma kwa Mlipakodi wa TRA Bw. Richard Kayombo amesema hii ni mara ya kumi na sita TRA inakutana na wafanyabiashara hao kutoka nchini China kwa lengo la kuwawezesha kufahamu mifumo ya kodi nchini.

Huduma za uwekezaji zinaenda sambamba na ushauri wa kisheria hususani zile zinazohusiana na masuala ya kodi kwa wageni kama anavyoeleza mwakilishi wa kampuni ya uwakili ya ABC Attorneys Bw. Sunday Godfrey.