Thursday , 27th Nov , 2014

Rais mstaafu wa awamu ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Benjamini Mkapa amesema vyuo vikuu nchini ni lazima viwe ni tanuri la kupika wasomi ili kuwaandaa watanzania kushindana katika soko la ajira katika dunia ya utandawazi.

Rais mstaafu wa awamu ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Benjamini Mkapa.

Mkapa amesema hayo mjini Iringa wakati akitunukiwa shahada ya heshima ya uzamifu ya sheria katika mahafali ya mwisho ya chuo kikuu kishiriki cha mtakatifu Augustino cha ruaha ruco, na kuongeza kuwa Changamot iliyopo kwa wasomi wa sasa ni ushindani katika Soko la Ajira.

Aidha Mkapa amewataka wasomi wa sasa kukabiliana na Changamoto hiyo watanzania wanapaswa kuwa wameandaliwa kikamilifu ili kumudu ushindani huo na wasomi hao wanatakiwa kutafuta njia nyingine ya kukabiliana na hali hiyo ikiwemo kujiari.

katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 1882 wametunukiwa
astashahada,stashada shahada ya uzamili katika fani mbalimbali ambapo mh mkapa amezindua pia kituo cha uhifadhi na utafiti wa mafunzo cha chuo hicho kitakachojulikana kama benjamin william mkapa resource center