Katibu Mkuu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi
Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya awali ya makadirio ya uwekezaji mwaka 2015 kimataifa iliyotolewa na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD, mwezi huu wa Januari ambapo kwa mujibu wa ripoti hiyo, mataifa mengi ya Afrika yameshuhudia kushuka kwa uwekezaji wa kigeni hususani yale ya Kusini mwa Sahara.
Katibu Mkuu wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi ametaja sababu za mataifa ya Afrika kusini mwa Sahara kukumbwa na hali hiyo inatoka na mataifa makubwa kuanza kujitoa katika nchi walizokuwa wanawekeza katika rasimali ya mafuta
Mataifa ya Afrika yaliyoko kaskazini kama vile Misri yalishuhudia kuongezeka kwa uwekezaji huku Marekani ndio kidedea katika nchi kumi zilizopata uwekezaji wa juu zaidi, nyingine ni China, Uingereza na Ufaransa ikichukua nafasi ya kumi.