Monday , 24th Jun , 2019

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Ruvuma, ameilishukuru Bunge la Tanzania kwa kupitisha Sheria ya utoaji wa mikopo ya asilimia kwa ya Mapato ya Halmashaui kwa Makundi ya kinamama Vijana pamoja na wenye ulemavu.

Mwenyekiti Raymond Mhenga ametoa kauli hiyo Mkoani Songea wakati alipokuwa akizungumza na Mtahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mjini Abdul Mjini kuhusiana na hali utekelezaji wa Sheria ya ugawaji wa mikopo kwa makundi maalum.

Akizungumza akiwa na Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM mkoa huo Mwenyekiti Henga amesema kuwa "nashukuru nimepata nafasi ya kukutana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea  Abdul Mshaweji pamoja na kushuhudia zoezi la utoaji wa Mikopo ya Sh milioni 61, ambazo ni 10% ya Fedha za mapato ya Manispaa kwa Makundi ya  wanawake,Vijana na Walemavu"       

"Niwaombe ndugu zangu mliopewa mikopo leo, Serikali inawajali sana hakikisheni mnaitumia kujikwamua kimaendeleo, na si kufanya mambo yasiyokuwa na msingi." amesema Raymond Mhenga