Balozi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Alvaro Rodgerz.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Filberto Sebregond na balozi wa umoja wa mataifa Alvaro Rodriguez wamesema hayo baada ya kutembelea miradi wanayoifadhili iliyopo ifakara wilayani Kilombero mkoani humo.
Mabalozi hao wamebainisha kuwa miradi inayosimamiwa na jumuiya hizo imekuwa ikilenga kuinua kipato cha wananchi wa Tanzania katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo pamoja na kuwajengea uwezo watu wa hali ya chini ili waweze kujikwamua na umaskini, sambamba na kusaidia nyanja mbalimbali za mawasiliano.
Baadhi ya wananchi walionufaika na miradi hiyo wakiwemo wakina mama wa ifakara walio wezeshwa katika shughuli za ujasiriamali, wamepongeza jitihada zinazoendelea kufanywa na jumuiya za kimataifa katika kuanzisha miradi na kutoa kipaumbele kwa kuendeleleza fursa za wananchi wa hali ya chini katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Aidha wajasiriamali hao wameomba uwezeshwaji zaidi wa upatikanaji wa masoko ya nje ya nchi ili waweze kujikwamua kupitia biashara za kimataifa.