Zeid Ra'ad al Hussein amesema kuwa unyanyasaji huo ulitokea baada ya shambulio la waasi katikati ya mwezi Disemba dhidi ya kambi tatu za kijeshi.
''Ishara zote ikiwemo kuongezeka kwa mgogoro wa kikabila zinaonyesha ushahidi'',alisema katika taarifa.
Burundi ipo katika hali ya sintofahamu kutokana na Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunzinza kujiongezea muda wa kuendelea kuongoza nchi hiyo.
Chanzo BBC

