ramani ya Marekani
Takwimu kutoka kituo cha taifa cha masuala ya afya zinaonesha kushuka kwa umri huo kwa wanaume kutoka miaka 76.5 mwaka 2014 na kufikia miaka 76.3 mwaka 2015.
Takwimu hizo zinaonyesha pia kuishuka kwa umri wa kuishi kwa wanawake kutoka miaka 81.3 mwaka 2014 mpaka kufikia miaka 81.2 mwaka 2015,
Pia zinaonesha kuongezeka kwa magonjwa yanayosababisha vifo kama magonjwa ya moyo, vifo kwa watoto wachanga na magonjwa mengine.
Kwa wastani umri wa kuishi nchini Marekani kwa sasa ni miaka 78.8 kwa wanaume na wanawake ikiwa ni 0.1 pungufu ikilinganishwa na mwaka 2014.