Ripoti ya utafiti uliofanywa na Thomas Scurfield, mchumi ambaye anafanya kazi na taasisi ya Natural Resource Governance Institute NRGI amesema jana jijini Dar es Salaam kwamba nchi za Ghana, Guine, Zambia, Sierra-Leon na Tanzania zinapoteza kati ya dola za kimarekani bilioni 100 mpaka 300 kwa mwaka kutokana na ukwepaji wa kulipa kodi.
Scurfield alitoa takwimu hizo wakati akiwasilisha ripoti ya utafiti wa uhamishaji wa bei katika sekta ya viwanda na jinsi ya kufahamu kilichopotea, utafiti uliofanyika katika nchi tano za kusini mwa jangwa la Sahara,katika hadhara iliyohudhuriwa na wadau kutoka serikalini, taasisi za kiraia na wanasheria.
Thomas Scurfield
Wakati akiwasilisha mchumi huyo alinukuu ripoti ya shirika la maendeleo ya biashara la umoja wa mataifa UNCTAD kwamba ukwepaji wa kulipa kodi ni moja ya changamoto kubwa na kuwa imechangiwa na uhamishaji wa sheria za bei katika nchi za viwanda na hasa nchi zenye madini.