Monday , 10th Nov , 2014

Serikali katika kisiwa cha Ukerewe cha Mkoani Mwanza wameanza taratibu za kuomba mikoa mingine kuwa hamishia baadhi ya wananchi kutoka katika kisiwa hicho.

Serikali katika kisiwa cha Ukerewe cha Mkoani Mwanza wameanza taratibu za kuomba mikoa mingine kuwa hamishia baadhi ya wananchi kutoka katika kisiwa hicho, kufuatia visiwa vyote 15 kati 38 vyenye makazi ya kudumumu kuanza kufurika watu hivyo wananchi kukosa sehemu za kulima na kukabiliwa na baa la njaa kila mara.

Ni katika mji wa Nansio Ukerewe jijini Mwanza ambapo baadhi ya wananchi wanalalamikia baadhi ya mila na desturi za makabila katika kisiwa hicho kuwa mbali na uzazi wa mpango, huku kisiwa hicho kikiwa na mwingiliano Mkubwa watu toka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi wanaoenda kisiwani humo kwa shughuli mbalimbali ikiwemo ununuzi wa samaki na dagaa hata uvuvi na wengine utalii.

Mkuu wilaya hiyo Bi Marry Onesmo anasema kuwa kila mara wilaya yake imekuwa ikikumbwa na baa la njaa kutokana na ardhi kuchoka huku ongezeko la watu likikua kwa kasi na kuacha ardhi ikibaki ileile ambapo anasema kuwa wilaya kupitia katibu tawala wa mkoa wananza taratibu za kuomba mikoa mingine kupokea wananchi kutoka kisiwa hicho na kuwapatia makazi ya kudumu.

EATV imefika katika hosipitali ya wilaya ya Ukerewe iliyopo katika mji wa Nansio, ambapo wananchi wanatoa kilio chao cha kukosa elimu juu ya uzazi wa mpango wala hamasa ya kujiunga na mifuko ya afya ya jamii CHF ili waweze kupata huduma bora za afya katika wiilaya hiyo.

Tags: