Saturday , 25th Oct , 2014

Kamati ya ufundi inayoshughulikia Oganizesheni ya Mikutano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi nchini Tanzania (UKAWA) imeandaa mkutano wa hadhara unaotarajiwa kufanyika Jumapili wiki hii katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya ufundi inayoshughulikia Oganaizesheni ya mikutano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi nchini Tanzania (UKAWA), Bw. Singo Benson Kigaila.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Singo Benson Kigaila amesema tayari wamesha fuata taratibu zote za kufanyika kwa mkutano huo wa hadhara ikiwemo kulitarifu jeshi la polisi na kwa kupitia mkutano huo UKAWA watatoa msimamo wao juu ya katiba pendekezwa.

Kigaila amesema viongozi wa UKAWA watatumia fursa ya mkutano huo pia kuelezea namna vyama hivyo visivyoridhishwa na maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi wa 12 mwaka huu.

Aidha Kigaila amesema kuwa umoja huo hauridhishwi na msimamo wa Serikali wa kupendekeza kura ya maoni kupigwa April 12 na kusema kuwa mpaka siku hiyo uboreshwaji wa dafari utakuwa bado haujakamilika.