Vijana wa Kitanzania wakiwa katika semina (Picha na Maktaba).
Kwa mujibu wa gazeti la Bild am Sonntag la Ujerumani mpango huo unaojulikana kama Ujerumani na Vijana wa Afrika umesanifiwa kushaajisha mabadilishano ya vijana katika Ofisi inayoshughulikia uhusiano wa Ujerumani na vijana wa Afrika.
Nchi za awali kuanza majaribio ya mpango huo ni Tanzania, Afrika Kusini na Benin.
Wizara ya ushirikiano wa maendeleo ya Ujerumani inataraji kupokea washiriki 400 kwa mwaka 2017 ambapo kuanzia Juni 30 vijana wanaweza kuanza kuomba kujiunga na mpango huo.