Friday , 15th Aug , 2014

Kutokana na kukua kwa sekta ya benki katika nchi za Afrika Mashariki, benki zilizo katika jumuiya hiyo zinatarajiwa kukua kwa aslimia 15 katika miaka miwili ijayo.

Ripoti ya takwimu za kiuchumi iliyofanywa na shirika la Moody Investment Services la nchini Marekani imesema ukuaji huo pia utachangiwa na kuongezeka kwa matumizi ya huduma za kibenki kwa wananchi.

Aidha ripoti hiyo imebainisha kuwa Pato la taifa katika nchi za EAC litakua kwa kwango cha juu kutokana na msukumo mkubwa katika kukua na kupanuka kwa sekta hiyo unaotokana na kuchangia pato la Taifa.

Wakati huo huo shirika la fedha la kimataifa IMF limetabiri ukuaji wa pato la taifa kwa nchi za EAC utaongezeka kutoka asilimia 6.6 mwaka 2012 hadi asiliamia 6.7 mwaka 2015.