
Bonnah ameyasema hayo alipokuwa akifanya mazungumzo katika kipindi cha HOTMIX kinachorushwa na EATV na kusisitiza kuwa Jiji la Dar es salaam lina miondombinu mibovu sana ya elimu hasa katika kipindi hiki cha elimu bure ambapo wanafunzi wengi wameandikishwa kwa wingi wakati miondombinu bado sii rafiki.
Katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kutoa elimu bure Mbunge huyo ameanzisha harambee ya kuchangia elimu katika jimbo lake na kuwezesha kupatikana kwa madawati katika baadhi ya shule, ukarabati wa miondombinu na kwa sasa anatengeneza gari la kuwezesha wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi waweze kusoma kwa kufanya majaribio kwa kutumia vifaa vitakavyofungwa katika gari hilo (mobile laboratory)
Aidha Mbunge huyo amesema jimbo lake linakabiliwa na changamoto nyingi za maji, barabara, ajira kwa vijana na suala la afya ila kwa sasa amejikita katika kuhakikisha elimu inakuwa na ufabnisi katika jimbo lake.
