Wednesday , 12th Aug , 2015

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk, Jakaya Kikwete, jana amefungua kikao cha kamati kuu ya halmsahuri kuu ya chama hicho huku akiwataka wajumbe wa kikao hicho kufanya kazi ya kupitia uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge kwa umakini.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk, Jakaya Kikwete

Akifungua kikao hicho Dk Kikwete amesema watu wengi kwa sasa wanasubiri kwa hamu kujua nani atakayesimama katika majimbo hayo.

Amesema jana na leo wanapaswa kumaliza kazi hiyo ili ibaki kuimba iyena iyena na CCM namba moja.

Awali akimkaribisha Dk, Kikwete, Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana amesema akidi ya wajumbe wa kikao hicho imetimia.

Amesema wajumbe wote wa CC ni 32 na waliohudhuria ni 25.

Vikao vya uteuzi ngazi ya Taifa vilianza rasmi siku ya jumamosi ambapo kilianza kikao cha sekretarieti kilichoketi kwa wiki mbili na kufuatiwa na kikao cha kamati ya usalama na maadili kilichokutana jana kwa siku moja.