Saturday , 5th Dec , 2015

Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania TRA imesema kwamba imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 7 ambazo hazikukusanywa kufuatia kupotea kwa makontaina 329 kutoka Bandari Kavu zilizopo jijini Dar es salaam.

Akiongea na vyombo vya habari jana Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA Dakta Phillip Mpango amesema makampuni 43 ambayo ameyataja yalikwepa kulipa kodi kutoka katika Bandari kavu yaani ICD inayomilikiwa na Mfanya biashara Said Salim Bakhresa na Kampuni yake.

Alhamisi iliyopita Rais Dakta John Pombe Magufuli alitoa siku saba kwa wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari na baada ya muda huo kupita hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mfanyabiadhara ambaye atabainika kukwepa kulipa kodi.