Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa TRA Bw. Richard Kayombo amesema, serikali aitatoza asimilia 18 ya VAT kwenye amana ya mteja wala haitatoza kwenye kiwango cha pesa kinachotumwa na mteja na badala yake asilimia 18 itatozwa kutokana na huduma iliyofanyika katika miamala hiyo.
Bw. Kayombo amewataka wananchi kutambua kuwa hii ni mara ya kwanza kwa serikali kutoza kiwango hicho cha fedha kama kodi kwenye huduma zitolewazo na mabenki na mitandao ya simu na kuongeza kuwa hatua hiyo itaongeza kiwango cha mapato yatokanayo na kodi.

