Wednesday , 13th Apr , 2016

Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Neema Rusibamaila, amesema kuwa tatizo la wanawake kutojifungulia hospitalini bado ni kubwa

hasa maeneo ya vijijini ambapo watu wanaamini kujifungulia nyumbani ndio ushujaa.

Dkt. Rusibamaila ametoa kauli hiyo hii leo kwenye mkutano uliowakutanisha waganga wakuu wa mikoa na wizara za afya kutoka nchi mbalimbali za Afrika na kuongeza kuwa hali hiyo inapelekea wanawake wengi kupoteza maisha pale wanapopata matatizo wakati wa kujifungua ambayo wangeweza kupata msaada Hospitalini.

Aidha, Dkt. Rusibamaila ameongeza kuwa serikali inaandaa utaratibu wa kila hospitali na vituo vya afya kuwa na huduma za upasuaji ili kuwasaidia wanawake watakaopata matatizo yoyote wakati wa kujifungua hospitalini.