Wednesday , 28th May , 2014

Idadi ya watu wanaofariki kutokana na ajali za barabarani kwa mwaka katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania ni kubwa ambapo takwimu zinaonyesha watu milioni sita hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ajali za barabarani.

Nguvu kazi muhimu kwa maendeleo ya nchi, hupotea kupitia ajali za barabarani kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu.

Hayo yameelezwa leo, Jijini Dar es Salaam na Daktari Bingwa wa Mifupa kutoka Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili, MOI Dkt. Edmund Ndalama wakati wa mkutano wa pamoja wa madaktari bingwa wa mifupa kutoka nchi za Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika.

Dkt. Ndalama asema madaktari bado wanahitaji kupata mafunzo ya namna ya kumsaidia mtu aliyepata ajali na kuumia vibaya ili kumsaidia kuokoa maisha yake na kupunguza vifo vitokananavyo na ajali za barabarani ambapo wengi wao kutoka katika nchi za Afrika wanapoteza maisha na kupata ulemavu kutokana na ajali za pikipiki marufufu kama Bodaboda.